
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Kenya: Familia hatarini kutokana na kupanda kwa kiwango cha maji ziwa Naivasha
Familia katika kijiji cha Kihoto mjini Naivasha, zimeendelea kutaabika kutokana na athari za kupanda kwa kiwango cha maji kwenye ziwa Naivasha, na kusababisha maji kuingia kwenye kijiji ambayo pia yamesababisha kuenea kwa magugumaji. Nikurejesha nchini kenya, katika eneo la bonde la ufa, ziwa Bogoria, ziwa Baringo na Ziwa Niavasha, ni mfano wa maziwa ambayo yameendelea kushuhudia kupanda kwa kina cha maji ndani ya miaka 10 zilizopita, katika eneo la Afrika mashariki.

